NAMBA 13 YA KAMUSOKO NI KAMA ILE YA MICHAEL BALLACK? - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 23, 2016

NAMBA 13 YA KAMUSOKO NI KAMA ILE YA MICHAEL BALLACK?


Mataji 15 tofauti ambayo kiungo wa zamani wa Ujerumani na klabu za Kaiserslauten, Bayer 04 Leverkusen, FC Bayarn Munich na Chelsea, Michael Ballack aliyashinda wakati wake wa uchezaji hakuna hata taji moja la kimataifa.

Achana na medali kadhaa alizoshinda kama mshindi wa pili, Ballack aliyekuwa akivaa jezi namba 13 ameshindwa katika michezo mitano ya fainali. Mechi 3 akiwa mchezaji kiongozi wa Ujerumani na fainali mbili za ligi ya mabingwa Ulaya. Baada ya kushinda taji la Bundesliga akiwa kinda wa Kaiserslauten msimu wa 1997/98, Ballack alitazamwa kama mchezaji bora kijana katika soka la Ujerumani.

Alipoteza mchezo wake wa kwanza muhimu wa kimataifa Mei, 2002 baada ya timu yake, Bayer Leverkusen kupoteza mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. Julai, 2002 akiwa ameifungia Ujerumani goli pekee katika game ya robo fainali na nusu fainali, Ballack akiwa anatumikia adhabu ya kadi mbili za manjano alishuhudia nchi yake ikipoteza game ya fainali ya kombe la dunia mbele ya Brazil.

Ndani ya muda usiozidi miezi miwili, Ballack alikuwa amepoteza mataji matatu makubwa huku mawili yakiwa ya kimataifa. Leverkusen ilipoteza uongozi wa muda mrefu katika ligi ya Bundesliga na kushuhudia Bayern Munich wakitwaa taji siku ya mwisho ya msimu wa 2001/02.

Miaka mitatu (2005) baadae, safari hii akiwa nahodha wa Ujerumani alishuhudia timu yake ikipoteza uongozi wa mchezo wa fainali wa FIFA Confederation Cup mbele ya Brazil. Tena katika ardhi yao. ‘Mzimu mbaya’ wa kupoteza game za fainali ulijirudia tena msimu wa 2007/08 na Ballack alipoteza fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya pili kufuatia Chelsea kupoteza mbele ya Manchester United kwa changamoto ya mikwaju ya penalti Mei, 2008.

Mwezi Julai, 2008 akiwa nahodha wa Ujerumani alishindwa kuzuia kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Hispania katika mchezo wa fainali ya mataifa ya Ulaya ‘Euro 2008.’ Mshindi huyo wa mataji manne ya Bundesliga na moja la ligi kuu England alikuwa kiungo mahiri mgumu wa kati.

Ubora wake katikati ya uwanja ulichangia kwa kiasi kikubwa kuitangaza jezi namba 13, na wachezaji wengi vijana walipenda kuitumia namba hiyo kuanzia miaka ya 2002. Akiwa mshindi wa Bundesliga mara nne, na mara moja akishinda taji la ligi kuu England, Ballack ni ‘mshindwa binafsi wa kimataifa’ na si namba yake 13 aliyokuwa akipendelea kuivaa.

Baada ya kupata maumivu siku chache kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010, Ballack aliondolewa katika timu ya Ujerumani na ni hapo jezi namba 13 ikafungua ukurasa mpya. Kutoka ‘jezi ya gundu’ hadi kuwa ya ‘mshindi wa kombe la dunia’ huku akifunga magoli 10 katika game 13 za michuano hiyo mikubwa zaidi ya kandanda duniani.

Akifunga magoli matano katika game 6 mwaka 2010 pale Afrika Kusini, Mueller akiwa kinda wa miaka 20 aliisaidia Ujerumani kufika nusu fainali kisha kushinda nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia. Miaka minne baadae akiwa na jezi namba 13 alicheza fainali yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na jezi namba 13 na kuisaidia Ujerumani kushinda ubingwa wa kombe la dunia 2014 nchini Brazil.

Kiungo ‘maestro’ wa Yanga SC raia wa Zimbabwe, Thaban Kamusoko ameshinda mataji ya ndani ya Tanzania akitumia zeji namba 13. Taji la ligi kuu bara msimu wa 2015/16 na lile la FA yameambatana na kiwango cha juu kiuchezaji.

Akiichezesha timu, akifunga magoli muhimu, na kukaba na kupiga pasi za mwisho zenye mwelekeo. Kamusoko ni kiungo mgumu na fundi ambaye hajawahi kuniangusha tangu alipojiunga na Yanga, Julai 1, 2015 akitokea FC Platnum ya kwao Zimbabwe.

Kuelekea game ya pili katika CAF Confederations Cup dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, Juni 28 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kamusoko, 28 anatazamiwa kukutana na kiungo mwingine fundi raia wa Zambia, Rainford Kalaba ambaye huvaa jezi namba 18. Jezi iliyotambulishwa na fundi wa zamani wa England na Manchester United, Paul Scholes.

Ushindi akiwa tayari ameshinda michezo ya Ngao ya Jamii na FA Cup, Kamusoko bado hajawa mshindi wa kimataifa lakini jezi yake haina gundu kama ile ya Ballack. ina bahati kama ile ya Mueller.

Man-Kamusoko v Kalaba nani atateka dimba la kati pale Taifa? Namba 13 ya Kamusoko si kama ile ya Michael Ballack vs Kalaba mwenye namba 18.

Kiasi itanikumbusha fainali ya Moscow, Mei 21, 2008 ambayo nilishuhudia Ballack akimtawala Scholes lakini ‘akishindwa kibahati.’ Mbinu, ufundi, maarifa binafsi, makombora ya mbali yenye uelekeo, tutarajie Yanga vs TP Mazembe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here