ITALY IMEIVUA SPAIN UBINGWA WA ULAYA - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, June 27, 2016

ITALY IMEIVUA SPAIN UBINGWA WA ULAYA


Baada ya kufahamika kuwa Italy itacheza dhidi ya Hispania, wengi walikuwa wakiihurumia The Azzurri.

Kabla ya kufuzu hatua ya 16 bora, Italy imaliza kama kinara wa Kundi E na walionekana kuwa ni kikosi bora kwenye michuano hii baada ya kuilaza Ubelguji pamoja na Sweden.

Antonio Conte alizawadiwa kukutana na mabingwa mara mbili wa Ulaya kikosi chenye wachezaji bora wa muda wote.

Ulikuwa ni uwezo binafsi wa golikipa wa Hispania David De Gea uliosaidia kupunguza idadi ya magoli.

Kama alivyofanya kwenye timu yake ya Manchester United, De Gea alikuwa muhimili muhimu kwenye timu yake kwa kuokoa michomo kadhaa ya waitaliano kwenye vipindi vyote vya mchezo huo wa 16 bora ya michuano ya Euro 2016.

Italy wangeweza kupata ushindi wa zaidi ya magoli 2-0.

Giorgio Chiellini na Graziano Pellewalifunga magoli huku Gianluigi Buffon akilinda vema nyavu zake lakini timu ya Italy ilifanya kweli katika pambano hilo.

Kipigo hicho kinaacha wengi wakiamini huo ndiyo mwisho wa Vicente Del Bosque. Lakini pia inaonekana licha ya kuwa ni mwisho wa VDB, Andres Iniesta na David Silva huenda nao pia wakaamua kuachana na timu ya taifa.

Italy sasa itakutana uso kwa uso na timu ya taifa ya Ujerumani.

Rekodi zilizowekwa
  • Italy imemaliza uteja wa kucheza mechi tano bila ushindi dhidi ya Spain (L2 D3) na imewafunga kwa mara ya kwanza tangu August 2011.
  • Huo ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa Italy dhidi ya Spain kwenye mchezo wa kimashindano tangu mwaka 1994 kwenye michuano ya kombe la dunia (2-1 kwenye robo fainali)
  • Spain imepoteza mechi nne kati ya saba zilizopita (W3 D0 L4) kwenye michuano mikubwa hii ni baada ya kucheza michezo 12 bila kupoteza (W10 D2 L0).
  • Magoli matatu kati ya matano ya Italy kwenye michuano ya Euro 2016 yamefungwa kuanzia dakika ya 88 na kuendelea.
  • Goli la Chiellini lilikuwa ni la kwanza kwa Spain kuruhusu kwenye hatua ya mtoano kwenye michuano mikubwa ya kimataifa tangu mwaka 2006 dhidi ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here