JE MKOSI WA ENGLAND KWENYE PENATI UTARUDI TENA DHIDI YA ICELAND - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, June 27, 2016

JE MKOSI WA ENGLAND KWENYE PENATI UTARUDI TENA DHIDI YA ICELAND

Sekela

England amerudi tena kwenye hatua ya mtoano ya michuano mikubwa na jambo hilo mara nyingi humaanisha kitu kimoja, Wananafasi kubwa sana ya kwenda kwenye mikwaju ya Penati.

Hii ni habari mbaya kwa waingereza.

England imepoteza kwenye hatua ya mikwaju ya penati mara 6 kati ya 7 aliyoshiriki tangu mwaka 1990, mpaka sasa watu wameanza kuona suala hili kama utamaduni wa timu ya England.

Wachezaji kama Stuart Peace, Chris Waddle, Gareth Southgte na David Batty wanakumbukwa zaidi kwa kukosa penati wakiichezea England kushinda kitu kingine walichofanya kwenye mpira. Hata wakina David Beckham nao pia wamekumbwa na janga hili.

England inacheza na Iceland kwenye hatua ya 16 leo Jumatatu June 27 mjini Nice na nahodha wao Wayne Rooney amesema kwamba timu yao imekuwa ikifanya mazoezi ya penati kila waendapo mazoezini Ufaransa, tena wakijaribu kufanya yaleyale watakaofanya kwenye mechi.

“Tunafanya yaleyale tutakayoyafanya kwenye mechi,” alisema Rooney “Japo ni tofauti kwa sababu ya mashabiki na presha iliyokuwepo kwenye mechi, lakini ni muhimu kwa wachezaji wetu kufanya mazoezi ya penati vilevile watavyozipiga kwenye mechi.”

Mazoezini Rooney amekuwa akiwaambia magolikipa upande gani atapiga penati zake ili kujizidishia ugumu

“Kama akishindwa kuidaka alafu anajua upande gani napiga basi hapo hamna tatizo,” alisema Rooney

Historia mbaya ya penati kwa timu ya England ilianza kwenye kombe la Dunia la mwaka 1990 ambapo mchezaji Pearce alipata bahati mbaya ya kuona penati yake ikidakwa na baadaye kidogo Waddle kupaisha penati yake juu kabisa katika kichapo cha nusu fainali dhidi ya Ujerumani.

Katika Euro ya 1996 ambayo England waliichezea nyumbani, timu hiyo ilimfunga Spain kwa penati kwenye robo fainali na Stuart Pearce aliweza kufunga penati moja na kwa kufanya hivyo aliweza kurekebisha makosa yake kwa kiasi kidogo. Lakini England walifungwa kwenye nusu fainali tena dhidi ya Ujerumani.

England walifungwa kwa Penati tena na Argentina kwenye hatua ya 16 ya kombe la Dunia la mwaka 1998, na walifanyiwa hivyohivyo na timu ya Ureno mara mbili mfululizo kwenye Robo fainali ya Euro 2004 na Kombe la Dunia la mwaka 2006.

Haikushangaza wengi England walipochapwa tena kwa penati dhidi ya timu ya Italy kwenye Robo fainali ya Euro 2012, huku wengi wakikumbuka ‘chip’ ya Andrea Pirlo dhidi ya Joe Hart.

Rooney alifunga Penati ya yake dhidi ya Italy lakini Ashley Young na Ashley Cole walishindwa kumfunga Gianluigi Buffon na wakahakikisha kuwa England wanaaga michuano hiyo kwa style yao iliyozoeleka.

“Kitu kizuri kuhusu kikosi chetu cha sasa ni kwamba sidhani kwamba kuna mchezaji ambaye alishawahi kupiga mkwaju wa Penati na kukosa kwa ajili ya England. Kwa hiyo kitu hicho hakitokuwa mzigo kwa mchezaji yeyote,” Rooney pia alielezea fikra zake na michezo inayochezeka pale mechi inapoenda penati

“Nakumbuka dhidi ya Italy nilikuwa nikifikiri ‘Najua napiga wapi Penati yangu’ na Buffon alikuwa akinyoosha kidole upande mmoja akiniambia kuwa anajua ninapopiga. Alikuwa sahihi.” Rooney alikumbuka huku akicheka “kwa hiyo na mimi nikaanza kufikria ‘nipige hukohuko au nipige pengine?’.Lakini mwisho wa siku niliamua kupiga upande wangu uleule na yeye akaruka upande mwingine.

“Yani kitendo cha kipa kukuoneshea upande mmoja tu, kinaweza kikakuchanganya kabisa yani. Ni kitu kigumu.”

Waingereza watakuwa wanaomba sana kwamba mechi yao dhidi yao Iceland isiende penati. Nchi hii ndogo ya watu 330,000 imeonesha uwezo mkubwa wa kukaba kwenye michuano hii na haitokuwa kitu cha ajabu mechi hii ikienda penati.

Iceland wameshangaza wengi kwenye michuano hii wakiwa bado hawajafungwa mpaka dakika hii na kumaliza juu ya Portugal kwenye kundi lao.

Rooney aliaangalia mechi ambayo Iceland walimfunga Uholanzi na kufuzu kwa ajili ya Euro 2016.

“Walikuwa wamejipanga sana na ilikuwa ngumu kutengeneza nafasi dhidi yao sawa na timu tulizokutana nazo tayari kwenye michuano hii,” alisema Rooney alipokuwa akizungmzia mechi za England dhidi ya timu za Slovakia, Russia na Wales.” Najua itakuwa mechi ngumu kwetu sisi na itakuwa ngumu kuwafungua na ndiyo maana tunabidi tucheze kwa spidi kubwa na kuwafanya wafanye kazi ili tuwachoshe na tuchukue nafasi zetu zitakapo kuja.”

Na suala hilo ndilo tatizo kubwa la timu ya England kwenye michuano hii aonavyo Rooney

“Tunabidi tuzidishe ukatili golini, tukipata nafasi tunabidi tuziweke zingine golini,” alisema mfungaji huyu bora wa timu ya England aliyefunga mmagoli 52 kwa nchi yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here