JPM- MA-DC NILIOWAACHA HAWAKUKIDHI VIWANGO - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 30, 2016

JPM- MA-DC NILIOWAACHA HAWAKUKIDHI VIWANGO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kwamba wakuu wa wilaya ambao walikuwa wakifanya kazi hiyo katika maeneo mbalimbali na kuachwa katika uteuzi wake maana yake hawakukidhi vigezo vinavyotakiwa.

Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakuu wa wilaya aliowateua hivi karibuni ambapo wakuuu wa wilaya 139 waliteuliwa huku wengi wakiachwa katika uteuzi huo na nafasi zao kuzibwa na watu wengine.Rais Dkt. Magufuli amesema uteuzi huo umezingatia vigezo vya uwajibkaji na uchapaji kazi katika maeneo yao, hivyo walioachwa hawakufanya vizuri inavyotakiwa.

‘’Wakuu wa wilaya tulioachwa hawakufikia vigezo tulivyokuwa tunavitaka pia tumechukua wakurugenzi 22 waliofanya vizuri katika wilaya zao’’- Amesema Rais Dkt. Magufuli.

Aidha Rais amewataka wakuu hao wa wilaya kuchapa kazi na kutumia mamlaka yao vizuri ili kuweza kuweza kutatua kero za wananchi na kuhakikisha haki ili waweze kumuwakilisha vyema katika nafasi hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here