Baadhi ya viongozi wa umoja wa ulaya katika mkutano wa hali ya juu Brussels
Shirikisha
Viongozi wa Ulaya wamemaliza mkutano muhimu huko Brusssels na kuwapa Uingereza ujumbe wa wazi kuendelea na hatua ya kujitoa kwenye umoja huo na wasitegemee upendeleo wowote, lakini wakipata taabu jinsi ya kuendelea mbele katika mpango usio na umaarufu huko Ulaya.
“Kuna watu wengi ulaya ambao hawafurahishwi na hali inayoendelea na kututarajia sisi kufanya bora vizuri alisema rais wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk wakati wa kikao cha mwisho katika mji mkuu wa Belgium Jumatano akiongeza kwamba viongozi watakutana tena mwezi September kuzungumzia hatua zijazo baada ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.
Mazungumzo ya Jumanne na Jumatano yalikuwa ya aina yake wakati umoja wa Ulaya ulipojaribu kujiweka sawa baada ya kujitoa kwa Uingereza ambako kumepelekea mvutano katika masoko ya fedha na siasa za Uingereza na kupelekea kujitafakari kwa kina juu ya kujipanga upya kwa jumuiya hiyo ya nchi 28.
No comments:
Post a Comment