Mgogoro baina ya wafugaji na wakulima Manyara. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, June 28, 2016

Mgogoro baina ya wafugaji na wakulima Manyara.


Mgogoro baina ya wafugaji na wakulima katika kata ya Qash wilayani Babati mkoani Manyara umechukua sura mpya baada ya wananchi kudai kuwa kuondolewa kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Crispin Meela utasababisha mgogoro huo kutomalizika kwa wakati kama ambavyo walitarajia.

Wananchi hawa wamesemakuwa mgogoro huo umedum kwa zaidi ya miaka kumi kutokana na utaratibu wa kuhamishwa kwa baadhi ya viongozi wa wilaya hii ambao kila wanapotaka kuchukua hatua ya kiutatuzi huishia kuondolewa bila muafaka kufikiwa.

Aidha, wananchi hawa wameeleza kukutana na vitisho pamoja na manyanyaso ya kunyang’anywa ardhi na baadhi ya watu wenye uwezo mkubwa kifedha.

Kati hii ndipo ulipogunduliwa uwepo wa uwanja hewa wa ndege ambao hata hivyo mwekezaji wake kutoka kampuni ya Quality Food Products anatiliwa mashaka na wakazi wa eneo hili kusafirisha wanya ma pori kutoka katika hifadhi hususani hifadhi ya tarangire uliopo jirani na uwanja huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here