Nguli wa soka wa Argentina Diego Maradona amewataka mashabiki wa soka kuacha kumsumbua Lionel Messi baada ya maamuzi yake ya kuamua kustaafu soka katika timu ya taifa.
Messi ametangaza kustaafu soka baada ya timu ya taifa ya Argentina kupoteza fainali ya tatu katika miaka mitatu baada ya kufungwa na Chile 4-2 kwa mikwaju ya penalty katika mchezo wa fainali ya Copa America Centenario.
Ilikuwa ni mara ya nne kwa Messi kufungwa katika mchezo wa fainali katika mashindano makubwa, ikiwa ni pamoja na mashindano ya mwaka 2007 na 2015 ya Copa, pamoja na fainali za kombe la Dunia mwaka 2014 ambapo walifungwa fainali na Ujerumani.
.
Maamuzi ya Messi yamewafanya mashabiki wengi wa Bara la Amerika Kusini kutokwa na machozi ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa serikali akiwemo raisi wa Argentina akimuomba Messi abatilishe maamuzi yake na kurejea uwanjani kuitumikia timu ya taifa.
Hata hivyo Maradona ambaye alishinda kombe la Dunia akiwa na Argentina mwaka 1986 amesisitiza kuwa watu wanapaswa kumuacha Messi kwa wakati huu.
"Messi anatuambia kuacha kuusema mpira wake," Maradona.
"hii ni sawa na Messi kutuambia kwamba anakwenda mapumziko, niacheni na wakati mtakaponiita nitafikiria. Sitaki kulizungumzia hili zaidi'. Anasema Maradona
No comments:
Post a Comment