TANZIA. VILIO VYATAWALA KITIVO CHA ELIMU CHUO KIKUU CHA DODOMA - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 30, 2016

TANZIA. VILIO VYATAWALA KITIVO CHA ELIMU CHUO KIKUU CHA DODOMA


Ikiwa ni mwezi mmoja umepita tangu wanafunzi wa Stashahada ya Elimu maalumu ya sayansi (Sekondari na Msingi) wa chuo kikuu cha Dodoma kukumbana na kile kilichoitwa uamuzi wa serikali kuondoka chuoni hapo haraka iwezekanavyo na kuleta taswira tata miongoni mwa wanafunzi na jamii kwa ujumla, wakati hayo yakiendelea kujiri na kugonga vichwa vya watanzania na wapenda maendeleo ya nchi hasa wale wadau wa Elimu, SIMANZI yaanza kutawala miongoni mwao mara baada ya tukio la kuondokewa na wanafunzi wawili waliotangulia mbele ya HAKI huku matukio hayo yakishabihishwa na msongo wa mawazo.

Spika mteule wa Bunge la Kitivo cha Elimu (Coed) Ndugu Gibson Johnson E. ( ambaye naye alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika stashahada hiyo) amewaelezea wanachuo kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna wanachuo wawili miongoni mwa waliokuwa wanafunzi wa special diploma waliorudishwa nyumbani wamefariki Dunia.  Amenukuliwa akisema.......

"Mpaka sasa tuna taarifa kuwa ndugu zetu BENARD E. MWITA (ODPE 1st year wa kitivo cha Elimu) mwenyeji wa mkoa wa mara aliyekuwa anasoma mkondo wa AA sambamba na Ndg. MABULA MASUMBUKO (SDE 2nd year - kitivo cha Sayansi ya jamii) wametangulia mbele za haki huku ikisemekana kuwa vifo vyao vikishabihishwa na kadha iliyowapata.

Vifo hivyo vimepokelewa kwa masikitiko makubwa na huzuni miongoni mwa wanachuo wa Dodoma hasa wale wa Kitivo cha Elimu mara baada ya kuondokewa na ndugu zao hao.


MUNGU ALITOA NA MUNGU AMETWAA. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

AMEN!!!!!

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here