MKUU WA MKOA WA LINDI GODFREY ZAMBI AFUNGA MAGHALA YANAYONUNUA UFUTA CHINI YA BEI YA SHILINGI 2100 - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, June 19, 2016

MKUU WA MKOA WA LINDI GODFREY ZAMBI AFUNGA MAGHALA YANAYONUNUA UFUTA CHINI YA BEI YA SHILINGI 2100

 Godfrey Zambi

Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kuzuia mara moja wafanyabiashara wanaonunua Ufuta chini ya Bei Elekezi ya Shilingi 2100 kwa kilo, lengo likiwa kumpa mkulima bei bora ya mazao yake.

Agizo hilo limeambatana na kuzuia na kufunga Maghala mbalimbali wilayaniNachingwea na Ruangwa ambayo yalikuwa yakinunua zao hilo kwa bei ya shilingi 1600 na 1500 kwa Kilo.

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo, ikiwemo ile Ikiwemo inayotekelezwa na Mfuko wa Jamii Tasaf na utengezaji wa Madawati, Mkuu wa Mkoa huo amekuta baadhi ya vyama vya msingi vikinunua zao la Ufuta kwa ukiukwaji wa Agizo la Mkoa.

Kwa upande wao, baadhi ya wakulima wameonyesha kutoridhika na agizo hilo la Mkuu wa mkoa, kutokana na hali ngumu walizonazo, huku wengine wakipongeza hatua hiyo inayolenga kumfanya Mkulima auze zao hilo kwa tija.

Katika Ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo wa Lindi alifunga Maghala ya Kijiji Cha Nambalambala wilayani Nachingwea, Mbekenyera, Naunambe, Nangumbu na Nanganga Stesheni wilayani Ruangwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here