TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI , KUN’GATUKA UENYEKITI WA TAIFA WA CUF 13 Juni 2016.
** Tarehe 5 Agosti 2015 nilimuandikia barua Katibu Mkuu kumueleza uamuzi wangu wa kun’gatuku Uenyekiti wa Taifa .
** Tarehe 6 Agosti nilizungumza na waandishi wa habari kuhusu kun’gatuka kwangu na kueleza kuwa “Dhamira na nafsi yangu INANISUTA**
**Kuwa katika maamuzi yetu ya UKAWA tumeshindwa kuenzi na kuzingatia Tunu za Taifa za UTU, UZALENDO, UADIRIFU, UMOJA , UWAZI na UWAJIBIKAJI "".
** Rasimu ya KATIBA na MAUDHUI yake tumeyaweka kando. Walio ipinga Rasimu ya Katiba ya Wananchi ndani ya Bunge Maalum la Katiba ndiyo tunaamini wataturahisishia kushinda uchaguzi **
""Tumeshindwa kuongozwa na maadili.”
** Baada ya Uchaguzi Mkuu"" nilijitokeza kuzungumzia dhulma iliyotendeka Zanzibar ya kupora ushindi wa CUF wa kiti cha Urais""
.** Nilifanya hivyo kama mwanachama wa CUF na Mtanzania baada ya kuona hakuna kauli nzito iliyotolewa na viongozi wa Tanzania Bara dhidi ya dhuluma hiyo""
**Kwa muda nimekuwa nashauriwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa CUF Zanzibar na hasa Tanzania Bara nirejee kwenye uongozi wa Chama"" Nimetafakari sana ushauri huo na kutathmini hali ya kisiasa katika nchi yetu na kama bado nina mchango chanya katika Chama na nchi kwa ujumla""
**Kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar baada ya mgombea wa CUF kushinda uchaguzi huo kulingana na matokeo yaliyo thibitishwa na wasimamizi wa majimbo "54" ya Zanzibar kunaonyesha wazi CCM hawana lengo hata la “kujibaraguza” kuhusu kuheshimu matakwa ya wananchi na kujenga demokrasia ya kweli nchini Tanzania"".
**Bila haya, Mwenyekiti wa ZEC kafuta matokeo ya uchaguzi kinyume cha sheria " wakati Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) iliyakubali matokeo ya Zanzibar ya Rais wa Jamhuri na Wabunge kuwa ni halali" Uchaguzi wa ZEC na NEC umefanyika pamoja katika mazingira sawa sawa""
**Linalo nitisha zaidi ni namna CCM walivyopanga matokeo katika “Uchaguzi” wa tarehe 20 Machi 2016 na kutangaza ushindi wa kishindo wa majimbo yote "54" ya Uwalkilishi na ushindi wa Rais wa asilimia 91.4.""
** Wakati televisheni zilionyesha ushiriki mdogo sana wa wapiga kura ZEC ilitangaza bila haya kuwa Wazanzibari 341,865 sawa na asilimia 68 ya wananchi walioandikishwa kwenye Daftari la Wapiga Kura la ZEC wamepiga kura""
** Vyombo vya Dola vya Muungano vimetumiwa kuhakikisha CCM inabakia madarakani Zanzibar"" Bila shaka Wazanzibari wanahisi kuwa Dola ya Muungano ambayo kiuhalasia ni dola ya Tanganyika inawanyima haki ya kisiasa ya kuchagua viongozi wao",. Muungano unazidi kutetereka , Muungano wa mabavu hauna muelekeo mwema**
**Wananchi wengi wa Tanzania Bara wanaamini CUF ilishinda uchaguzi wa Zanzibar. Hata hivyo hakuna uhamasishaji wa kuwafahamisha Watanzania wa Bara ikiwa CCM hawaruhusu Wazanzibari kuchagua viongozi wao ni wazi hawataruhusu Watanzania kwa ujumla kupata Rais na Serikali ya Muungano isiyokuwa ya CCM",.
**Suala la kudai chaguo la Wazanzibari katika uchaguzi halali wa tarehe 25 Oktoba 2015 liheshimiwe linapaswa kuwa la Watanzania wote na siyo Wazanzibari peke yao.
Ni muhimu katika kipindi hiki kigumu kurejesha umoja wa kweli wa wana CUF. Sote tupambane dhidi ya kubakwa kwa demokrasia Zanzibar "
**Rais Magufuli ameingia kwa kishindo na kuteka agenda zetu za kupambana na RUSHWA na UFISADI, kusisitiza matumizi ya FEDHA za UMMA yenye tija, na ELIMU ya MSINGI na SEKONDARI ya bila malipo. Agenda ya DEMOKRASIA na HAKI kaiweka kando. Anaamini katika kuendesha nchi kwa ” ""KWATA KWATA".” Nchi inaelekea kwenye UDIKTETA""
**Kauli mbiu ya Haki SAWA KWA WOTE ina mvuto mkubwa kwa wananchi wa kawaida. Mvuto huo utaongezeka kwa kadri UDIKTETA wa SERIKALI utakavyodhihirika"". Tunahitaji UMOJA ndani ya Chama kuongoza MAPAMBANO ya KISIASA ya kujenga DEMOKRASIA ya kweli ZANZIBAR na TANZANIA kwa ujumla**
**Nawapongeza sana wote mliofanikisha KAMPENI mpaka tukashindaa majimbo kumi ya ubunge"". Tuzingatie kuwa kote tulikoshinda tulifanya kazi ya KISIASA ya muda mrefu. Kuna majimbo mengi TUMEPORWA**
.
**Kwa kuzingatia CHANGA MOTO za KISIASA zinazoikabili NCHI yetu na CHAMA chetu nimekubali rai ya VIONGOZI wa DINI, WANACHAMA na baadhi ya VIONGOZI nirejee kwenye UONGOZIi wa CHAMA"".
**Kwa kuwa BARUA yangu ya Tarehe 5 Agosti 2015 ilikuwa HAIJAJIBIWA, Nimemuandikia BARUA Katibu Mkuu KUTENGUA , BARUA yangu ya KUJIUDHURU na KUREJEA kwenye NAFASI yangu niliyo CHAGULIWA ya MWENYEKITI wa TAIFA""
Katibu Mkuu ANAISHUGHULIKIA barua hii kwa kupata ushauri wa WANASHERIA wetu wa Chama ili KATIBA ya Chama iheshimiwe""
Katika suala hili Ibara ya 117 ya Katiba inaeleza vizuri taratibu za kiongozi kujiuzulu. Ninanukuu Ibara ya " 117 "
“ 117." (1) Kiongozi yeyote wa chama anaweza kujiuzulu uongozi wake wakati wowote ule "
.
(2) Kiongozi ATAJIUZURU kwa kuandika BARUA na kuweka saini yake kwa KATIBU wa mamlaka "" ILIYO MCHAGUA au KUMTEUA"" na kiongozi huyo atahesabiwa kuwa AMEJIUZULU
ikifika tarehe aliyoainisha katika BARUA yake kuwa ATAJIUZULU"" PINDIPO akikubaliwa na mamlaka ILIYO MCHAGUA au ILIYO MTEUA"", au kama hakuainisha tarehe ya KUJIUZULU kwake basi atahesabiwa AMEJIUZULU "" mara baada ya KATIBU wa mamlaka iliyomteua au kumchagua kupokea barua hiyo na MAMLAKA ILIYO MCHAGUA au KUMTEUA kukubali.”"
**Mamlaka ILIYO NICHAGUA mimi ni MKUTANO MKUU"". Mkutano Mkuu bado HAUJA POKEA barua yangu. Kwa kuzingatia hali ya KISIASA nchini na USHAURI na NASAHA za VIONGOZI wa DINI, WANACHAMA naVIONGOZI wa CHAMA nimeamua KUTENGUA barua yangu ya KUJIUZULU".
Natoa RAI kwa WANACHAMA wote TUSHIKAMANE na kuwa na UMOJA wa DHATI katika kipindi KIGUMU.
Prof. IBRAHIM H. LIPUMBA
No comments:
Post a Comment