NDONDO CUP YAENDELEA KUPANDA THAMANI - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, June 19, 2016

NDONDO CUP YAENDELEA KUPANDA THAMANI


Na Yahaya Mohamed

Kampuni ya Mwananchi Communicanions Limited kupitia gazeti lake la Mwanaspoti, gazeti namba moja la michezo, imetia saini makubaliano ya kudhamini michuano ya Sports Extra Ndondo Cup.

Katika uzinduzi wa makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Mwananchi Communications LTD Francis Nanai amesema, pamoja na kudhamini kwa mara ya kwanza michuano hiyo, wamejipanga vilivyo kuhakikisha mchango wao kwa vijana unaonekana lakini kubwa zaidi ni kuhakikisha Ndondo Cup inachezwa inchi nzima.


“Tunajua michezo ni furaha michezo huleta umoja na mshikamano, yote hii inaleta taswira nzuri ya umoja katika taifa lolote. Sisi kama Mwananchi Communications tunaunga mkono umoja, furaha na kupendana, kwahiyo ni vizuri kuunga mkono Ndondo Cu.”

“Ndiyo tumeanza mwaka huu na hatujawahi ku-support mashindano haya lakini naimani kwamba mwaka kesho na miaka inayokuja kwa ruhusa ya waandaji tunaweza tukaenda hadi nje ya mkoa wa Dar es Salaam.”

“Mwananchi litakuwa linatoa matukio ya kila siku, picha, habari na maelezo, kwahiyo mashabiki, wachezaji na viongozi watajiona kwenye gazeti la Mwanaspoti la ambalo litakuwa likifatilia michuano ya Ndondo tu ‘Ndondo Cup Mwanaspoti’.”

Kwa upande wa Clouds Media Group ambao ndiyo waandaaji wa Ndondo Cup kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra, wanaipongeza kampuni ya Mwananchi Communications kupitia Mwanaspoti kwa kuiona fursa na kuamua kuwekeza katika michuano hiyo.

“Sisi Clouds Media Group, tunatoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Mwananchi. Mlengo wetu mkubwa ni vijana lakini pia tupo kwa ajili ya kuelimisha na kuzuia vitendo viovu mtaani kupitia mashindano haya


“Ukiangalia hizo pesa, kwa kiasi kikubwa zinakwenda kwa wenyewe (timu washiriki) na tumekuwa tukiwaambia kwamba kadiri siku zinavyosonga mbele wadau wataongezeka na mwisho wa siku sisi tutaona namna ya kuwatengenezea mazingira ya rahisi ya kucheza kwa utulivu,” amesema Shaffih Dauda ambaye ni mkuu wa vipindi wa Clouds Media Group.

Katika udhamini huo wenye thamani ya shilingi milioni 50 ambao utaanza kufanya kazi katika hatua ya 16 bora, katika kila mchezo atatafutwa mchezaji bora wa mchezo husika ambaye atafahamika kama mchezaji bora wa Mwanaspoti wa siku ambaye atapata shilingi 50,000.

Timu bora ya wiki itaambulia kitita cha shilingi 200,000 lakini kikundi bora cha ushangiliaji cha Mwanaspoti chenyewe kitapata shilingi 100,000 kwa wiki huku kukiwa na zawadi mbalimbali zikiwemo zile za mwisho wa mashindano ambapo zitaolewa pia kwa mabingwa, washindi wa pili, na washindi wa tatu.

Sasa ni wakati wa kuvuna kupitia Sports Extra Ndondo Cup.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here