‘TP MAZEMBE SI ILE YA SAMAGOAL, ILA YANGA MNAMJUA MTU HATARI KALABA? - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, June 22, 2016

‘TP MAZEMBE SI ILE YA SAMAGOAL, ILA YANGA MNAMJUA MTU HATARI KALABA?


Baada ya kupoteza game ya kwanza ugenini dhidi ya MO Bejaia ya Algeria siku ya Jumapili iliyopita, mabingwa wa Tanzania bara, Yanga SC watawakabili mabingwa mara tano wa kihistoria, timu ya TP Mazembe ya DR Congo, Juni 27 au 28 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kila aliyetazama pambano la Yanga na Bejaia atakuwa ameona mapungufu kadhaa katika timu hiyo hasa inapodhibitiwa katika sehemu za pembeni ya uwanja. Kama viungo wangetengeneza nafasi za kufunga Yanga wangeweza kufunga lakini si Haruna Niyonzima wala Thaban Kamusoko aliyeonekana kusogea na kujaribu kupiga kiki za mbali au pasi za juu wakati fulani.

Nilishasema sababu zilizochangia kuanguka kwa Yanga katika game iliyopita, lakini jambo lingine naanza kuligusia kuelekea game yao ya pili dhidi ya TP Mazembe kiuhalisia imeshuka kiwango, si timu ile iliyoshinda taji la Champions league miezi 7 iliyopita.

Lakini wanaye mchezaji bora zaidi wa nafasi ya kiungo anayecheza ndani ya Afrika. Rainford Kalaba, akiwa na miaka 29 hivi sasa mchezesha-timu huyu mfungaji wa timu ya Taifa ya Zambia ni mtu hatari zaidi kwa Yanga na si ajabu akawa ‘mtu wa mashabiki’ baada ya dakika 90′ dhidi ya Yanga.

Akiwa na uzoefu wa kucheza kwa mwaka mmoja katika timu ya pili ya Nice ya Ufaransa mwaka 2005 (miaka 11 iliyopita) miaka miwili katika timu ya SC Braga ya Ureno (2008-2010) na miaka 11 mfululizo kama mchezaji wa timu ya Taifa za Zambia ‘Chipolopolo,’ Kalaba ni mchezaji mwenye maarifa mengi binafsi, ana kasi, anapiga pasi na mashuti yenye mwelekeo golini, ana nguvu kiasi lakini si rahisi kumdhibiti.

Mshindi huyu wa Champions league (2015) mataji manne ya ligi ya DR Congo (2011, 2012, 2013, 2014) ni changamoto kubwa ijayo kwa viungo wa Yanga na ni lazima wajipange kumzima. Ikiwezekana kumzuia Kalaba asicheze kwa uhuru itakuwa ni sawa na ushindi upande wa Yanga na wataizima timu nzima ya Mazembe ambayo imeundwa kiuchezeshaji.

Yanga wanapaswa kumtazama mchezaji huyo ambaye alifunga magoli mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi Medeama ya Ghana katika game yao ya kwanza Stade de TP Mazembe. Anapiga pasi za kwenda mbele na makini katika umaliziaji.

Ni mchezaji anayekimbia kwenda mbele huku akijetengenea nafasi za kufunga na anapoipata huitumia vizuri. Anapenda sana kugeukia upande wa kushoto ili apate urahisi wa kushuti au kupiga pasi za mwisho. Si mchoyo hivyo hupiga pasi za haraka inapotokea ametazama nafasi iliyo wazi. Yanga ni lazima wamzime kwanza Kalaba ambaye anaweza kuinyanyua timu yake hata ikiwa katika nyakati ngumu mchezoni.

Mazembe ni kweli si ile timu iliyoshinda ubingwa wa mabingwa mwishoni mwa mwaka uliopita ikiwa na mfungaji bora, mchezaji bora wa michuano na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, Mtanzania, Mbwana Samatta ambaye sasa anakipiga KRC Genk ya Ubelgiji, ila katika kikosi cha wababe hao wa Afrika, amebaki mchezaji mbunifu mfungaji na mpiga pasi wa hatari zaidi, Kalaba.

ITAKUWA MECHI YA TOM…

Yanga haijawahi kucheza na Mazembe katika michuano ya CAF, lakini pia hawajawahi kukutana na mshambulizi kijana wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu. Kwa aina ya game, mazingira, Tom atacheza game hiyo ikiwa atakuwa timamu kimwili na kiakili.

Kama hilo litatokea, TP itabaki katika hadhi yake kama timu bingwa mara tano wa Champions league, tena wakitoka kushinda kwa mara ya mwisho miezi 7 iliyopita. Yanga wajiandae kumzima Kalaba, lakini jicho lao la tatu walitupe kwa Thomas Ulimwengu.

Kufungwa itamaanisha ‘michuano ni mikubwa kwao’ kimbinu, kiuwezo, na kiushindani, kwa maana Mazembe watafikisha alama 6 (ikiwa watashinda) na ikitokea Bejaia nayo kuifunga Medeama, kundi litakuwa wazi kwa washindani wa kundi. Ushindi utasimamisha kundi na kulirudisha katika usawa kwa wawakilishi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here