Spain itakutana na Italy kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016 baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika Kundi D kufuatia kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Croatia ambao wameongoza kundi hilo.
Spain walianza kupata bao la kuongoza lilifungwa na Alvaro Morata ambaye aliunganisha pasi ya Cesc Fabregas iliyoshindwa kuokolewa na golikipa wa Croatia Danijel Subasic.
Ivan Rakitic almanusura aisawazishie Croatia lakini mpira aliuou-chop uligonga mtambaa panya kabla ya kudakwa na David de Gea lakini Nikola Kalinic akaisawazishia Croatia kwa kuunganisha krosi ya Ivan Perisic.
Subasic aliokoa mkwaju wa penati iliyopigwa na Sergio Ramos wakati Perisic aliifungia Croatia bao la ushindi na kuikatia tiketi nchi yake kushiriki hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Bao la Perisic dakika ya 87 katika game iliyokuwa kali limeifanya Spain kupoteza mechi ya kwanza katika game 15 walizocheza kwenye michuano ya Ulaya.
Msimamo wa Kundi D baada ya mechi zao za mwisho huku Crotia ikakaa kileleni kuongoza kundi hilo baada ya ushindi dhidi ya Spain
Croatia watakipiga siku ya Jumapili mjini Lens wakati Spain wao Jumatatu watachuana dhidi ya Italy jijini Paris.
Je ulikuwa unatambua kwamba
Croatia watakipiga siku ya Jumapili mjini Lens wakati Spain wao Jumatatu watachuana dhidi ya Italy jijini Paris.
Je ulikuwa unatambua kwamba
Hii ni mara ya kwanza kwa Spain kupoteza mchezo kwenye fainali za Euro baada ya kuwa mbele ikiongoza kwa magoli.
Sergio Ramos ni mchezaji wa kwanza wa Spain kukosa penati kwenye michuano ya Ulaya tangu Raul alipokosa dhidi ya Ufaransa mwaka 2000.
Cesc Fabregas amehusika kwenye magoli mengi kuliko mchezaji yeyote wa Hispania katika fainali za Euro (magoli matatu na assists tano)
Video ya magoli yote ya mchezo wa Croatia vs Spain
No comments:
Post a Comment