Michuano ya Copa America kwa mwaka 2016 ndio inaelekea ukingoni, sasa umebaki mchezo wa fainali pekee kuhitimisha michuano hiyo, ambayo kwa mwaka 2016 imefanyika maalum kusherekea miaka 100 ya mashindano hayo toka yaanzishwe 1916.
June 26 2016 ilikuwa ni siku ambayo mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulichezwa kati ya USA dhidi ya Colombia, kabla ya mchezo huo Colombia alikuwa ana rekodi nzuri zaidi kuliko USA, kwani walikuwa wamekutana jumla ya mechi 19, USA ameshinda mechi tatu kati ya hizo na kupoteza 13.
Bado alfajiri ya June 26 iliendelea kuwa ngumu kwa USA, kwani wamekuabli kupoteza mchezo wa 14 dhidi ya Colombia kwa kukubali kufungwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Carlos Bacca dakika ya 31. Alfajiri ya June 27 ndio siku ambayo utachezwa mchezo wa fainali utaozikutanisha Argentina na Chile.
No comments:
Post a Comment