Bao la Ricardo Quaresma kwenye muda wa nyongeza limeipa ushindi Ureno na kuipeleka hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016 na itakutana na Poland kwenye mchezo war obo fainali.
Quaresma aliyetokea benchi alifunga kwa kichwa hatua mbili kutoka golini baada ya golikipa Danijel Subasic kuupangua mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo.
Pambano hilo lilibidi kwenda hadi dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Croatia ilikaribia kufunga magoli kupitia Domagoj Vida na Marcelo Brozovic kwa mipira ya vichwa wakati Ivan Perisic yeye shuti lake liligonga wamba.
Mchezo wa robo fainali wa Ureno utachezwa Alhamisi kwenye uwanja wa Stade Velodrome, Marseille.
Rekodi zilizowekwa
- Ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Ronaldo ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza kwenye michuano ya Ulaya kucheza dakika 90 bila kupiga shuti hata moja.
- historia ya michuano ya Euro kufunga magoli matatu akitokea benchi, alitanguliwa na Rui Costa na Helder Postiga.
- Quaresma amefunga goli la kwanza kwenye muda wa ziada kwenye mashindano ya Euro tangu Andrey Arshavin alivyofanya hivyo mwaka 2008 dhidi ya Uholanzi.
- Croatia ilipiga mashuti 17 lakini hakuna hata moja lililolenga goli. Hii ni timu iliyopiga mashuti mengi off target tangu mwaka 1980.
Video ya highlights za mchezo wa Ureno vs Croatia
No comments:
Post a Comment