Baada ya mechi 9, hatimaye Ujerumani yajivua uteja kwa Italy – mechi yao yaweka rekodi hii kubwa - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, July 2, 2016

Baada ya mechi 9, hatimaye Ujerumani yajivua uteja kwa Italy – mechi yao yaweka rekodi hii kubwa

Baada ya kujaribu kwa takribani mara 9 hatimaye usiku wa leo timu ya taifa ya Ujerumani imefanikiwa kuwafunga Italy katika mashindano makubwa na kufanikiwa kusonga mbele hadi nusu fainali ya michuano ya Euro 2016.


Timu hizo zilikwenda sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 na ilipofika hatua ya mikwaju ya penalti Ujerumani wakashinda 6-5.


Miamba hiyo ya soka barani Ulaya ililazimika kwenda hadi penalti ya tisa ndipo mshindi alipopatikana kwa Italia kupoteza jumla ya penalti nne huku Ujerumani wakipoteza tatu.


Ujerumani walipata bao la kuongoza dakika ya 65 kupitia kwa Mesut Ozil lakini Leonardo Bonucci akaisawazishia Italia kwa njia ya penalti dakika ya 78. 


Mchezo huu umeweka rekodi ya kuwa na mikwaju mingi ya penati zaidi katika kipindi cha miaka 36, zimepigwa jumla ya penati 18 – mara ya mwisho kwa mchezo wa Euro kuamuliwa na idadi kama hii ya penati ilikuwa mwaka 1980 wakati Italy walipofungwa 8-9 na CzechSlovakia.


Pia Ujerumani wameendelea kuwa na rekodi nzuri ya kutopoteza mechi kwa mikwaju ya penati kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita – historia inaonesha wamefanikiwa mikwaju mara 7 kati ya 8.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here