Habari iliyoripotiwa hivi punde na kituo cha ITV ni kuhusu ajali ambayo imetokea eneo la VETA DAKAWA mkoani Morogoro ikihusisha magari matatu ambayo ni lori la mafuta, kontena lililobeba mchele pamoja na basi.
Taarifa hiyo inasema kuwa watu 11 wamefariki dunia na wengine ambao idadi yao bado haijajulikana wamejeruhiwa.
Ajali hiyo imetokea wilaya ya KILOSA huku ikihusisha Bus la kampuni ya OTTA likitokea BUKOBA kuelekea D'SALAAM kugongana na loli la mafuta lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara.
Kuna abiria wamekufa ikiwajumuisha na madereva wote wawili na wasaidizi wao pamoja na abiria wengine.
Miili ya marehemu imekimbizwa na mingine bado inapelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa utambuzi na kwa itifaki ila mahututi wengine wanapatiwa matibabu hapo hospitali ya ST JOSEPH inayomiliikiwa na Kanisa la Roman Catholic.
Rai:Kama una ndugu unahisi au unafahamu alikuwa anasafiri basi fanya mawasiliano naye mapema. Sambaza taarifa hii katika magroup mengine.
Source ITV
No comments:
Post a Comment