Mtafiti wa kimataifa Bi Jane Goodall anatarajiwa kutunukiwa tuzo maalumu inayotambua mchango wake katika kuwalinda wanyama jamii ya sokwe walioko katika hatari ya kutoweka nchini Tanzania.
Bi Goodall amewezesha wanyama hao kuendelea kustawi katika hifadhi za taifa zaGombe na Mahale zilizopo kwatika mwambao wa ziwa Tanganyika, nchini Tanzania.
Mtafiti huyo mwenye asili ya Uingereza, alianza kazi hiyo mwaka 1960, ni miongoni mwa watu wanao aminika kutumia taaluma zao kuokoa wanyama walioko katika hatari ya kutoweka duniani.
Kwa sasa anaendelea kufanya utafiti wa wanyama nchini Tanzania na atapata tuzo na shirika la hifadhi za Tanzania (TANAPA).
Meneja mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete amesema hatua ya kutoa tuzo hiyo ni sehemu ya mikakati ya shirika hilo ya kuhakikisha linawashirikisha wadau mbalimbali katika uhifadhi kitaifa na kimataifa.
Bw Shelutete pia amewashauri wataalamu na watafiti wa Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika kutumia taaluma zao kusaidia masuala ya uhifadhi.
Kutokana na juhudi za Bi Jana Goodall idadi ya Sokwe imeongezeka katika hifadhi za Gombe na Mahale.
No comments:
Post a Comment