Sasa sio siri tena suala la mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic kujiunga na Manchester United.
Baada ya tetesi za siku hadi siku, lakini kilichokuwa kikisubiriwa ni uthibitisho tu kutoka kwa klabu au mchezaiji, na hilo limeshatokea.
Raia huyo wa Sweden ametangaza rasmi kupitia account yake ya Instagram na Twitter kwamba, mkataba wake na PSG umemalizika na mwisho wa siku alikuwa tayari kuthibitisha taarifa za kujiunga na Man United.
Wakati wote wa michuano ya Euro 2016, vyombo vya habari vilikuwa vikimhusisha Zlatan kuijiunga na United lakini hakuthibitisha hilo, yeye akasisitiza anahitaji kufikiria zaidi michuano ya Euro akiwa na timu yake ya Sweden.
Lakini kocha wake wa zamani Jose Mourinho akiwa boss mpya wa Old Trafford, ataungana na Zlatan kitu ambacho awali kilionekana kitakuwa kigumu lakini kilakitu kimeshatimia.
Zlatan anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kesho na baada ya hapo atatangazwa rasmi mbele ya waandishi wa habari akiwa kwenye uzi mwekundu.
Akiwa mchezaji huru, Zlatan atapatiwa mkataba wa mwaka mmoja kukipiga ndani ya Old Trafford.
No comments:
Post a Comment