Imebainika kwamba ushawishi wa kundi la Dola la Kiislamu Afrika Mashariki umeongezeka kwa kuwaandikisha vijana wa Kenya kuendesha mapambano ya jihadi nchi za nje na baadhi yao kurudi Kenya kuitishia nchi hiyo.
Mashirika ya ujasusi nchini Kenya yanakadiria kwamba takriban wanaume na wanawake 100 huenda wakawa wamekwenda kujiunga na kundi la Dola la Kiislamu nchini Libya na Syria na kuzusha hali ya wasi wasi kwamba baadhi yao wanaporudi nchini humo hufanya matukio ya kigaidi.
Rashid Abdi mchambuzi mwandamizi katika Shirika la Kimataifa la Kushughulikia Mizozo ambalo ni jopo la ushauri lilioko katika mji mkuu wa Kenya Nairobi amesema kwamba hivi sasa kuna tishio la kutoka kwa kundi hilo na kutoa tahadhari kwa vyombo vya usalama nchini humo.
No comments:
Post a Comment