MAELFU WAANDAMANA KUMUUNGA MKONO MUGABE. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, July 23, 2016

MAELFU WAANDAMANA KUMUUNGA MKONO MUGABE.


Na Leonard Msigwa/GPL
Maelfu ya wafuasi wa chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe wameandamana kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Harare, kwa lengo la kumuunga mkono Rais Mugabe aliyetawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 36.


Maandamano hayo yamekuja siku chache baada ya mlolongo wa matukio ya wapinzani wa kiongozi huyo mwenye miaka 92 kumtaka aachie madaraka. Wakilalamikia kushuka kwa uchumi, rushwa na uvunjifu wa haki za binadamu.


Mgomo kazini ulioitishwa kupitia mitandao ya kijamii na mchungaji Evan Mawarire, mapema mwezi huu umepata mwitikio mkubwa nchi nzima kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.


Rais Mugabe jana jumanne alimpinga mchungaji Mawarire kwa uwazi mbele ya halaiki huku akimtaja jina lake na kumwambia yeye na wafuasi wake wanaweza kuhama nchini Zimbabwe endapo wanaona hawana furaha kuishi nchini humo.


Wafuasi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kumuunga mkono kiongozi huyo wakiwa na mabango mbalimbali yenye picha zake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here