MAN UNITED YAPEWA KIPIGO CHA KWANZA CHINI MOURINHO .. MWENYEWE ATETEA TIMU YAKE. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, July 24, 2016

MAN UNITED YAPEWA KIPIGO CHA KWANZA CHINI MOURINHO .. MWENYEWE ATETEA TIMU YAKE.


Jose Mourinho amesisitiza kwamba hawezi kujaji wachezaji wake wa Manchester United kutokana na kipigo cha mabao 4-1 walichokipata kutoka kwa Borussia Dortmund na kusema kwamba: “Injini ilikuwepo ilikuwa ni tofauti kabisa, iliku ni kati ya Formula One against Formula Three”

“Mawazo yangu ni rahisi mno,” alisema Mourinho. “Najua kwamba wakati huu wa pre-season timu ambayo iko vizuri kwenye maandalizi lazima iwe vizuri zaidi ya Timu nyingine.”

“Hii hutokea kila mwaka. Baadhi ya timu bora hupoteza kwa magoli mengi. Nadhani hili lipo wazi kabisa. Baada ya dakika 10, tulianza kujua kwamba timu moja ilianza mazoezi siku 10 zilizopita na kucheza mchezo mmoja na nyingine ilianza mwezi mmoja uliopita na imeshacheza michezo minne. Ni rahisi mno kuona utofauti wa ugumu wa mchezo na umakini wa wachezaji. Kwa upande wetu ulikuwa ni mchezo mgumu sana.

Kipindi cha pili tulikuwa wazuri na kuuzoea zaidi mchezo. Nadhani matokeo ya mabao 3-2 yangekuwa sahihi zaidi ya 4-1 lakini Dortmund walionesha ubora mkubwa waliokuwa nao, kwa mchezaji mmoja-mmoja na timu nzima. Walionesha kwamba walikuwa wameshapiga hatua kubwa kwenye mazoezi zaidi yetu.

Alipoulizwa kama angewajaji wachezaji wake kutokana na mchezo ule, Mourinho akajibu: “Mimi nadhani ni muunganiko wa sababu vitu mbalimbali. Lakini kwa kuzungumzia uhalisia wenyewe, sidhani kama naweza kuwafanyia tathmini ilhali kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya timu hizi. Kwa sasa injini zina utofauti mkubwa. Formula One dhidi ya Formular Three.

‘Kwa sasa, wapo vizuri zaidi na unaweza kuona hilo kirahisi zaidi, hivyo ni vigumu sana kuwajaji wachezaji wangu. Hata kwenye masuala kama haya, unaweza kupata wachezaji watatu, wanne au watano. Vinginevyo ni vigumu sana japo unaweza kuona ubora uliopo.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here