MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI CAG AFICHUA JIPU LA KUTISHA. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, July 2, 2016

MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI CAG AFICHUA JIPU LA KUTISHA.


Ni jipu. Ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kusema halmashauri 34 nchini zimetumia Sh1.45 trilioni za miradi kugharimia shughuli ambazo hazikuwamo kwenye bajeti.

Profesa Assad ameyasema hayo katika mafunzo yaliyotolewa kwa watu wa kada mbalimbali kuhusu Toleo la Vijarida Maalumu vya Wananchi kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni mwaka 2014 na kukusanya maoni ya ripoti ya CAG.

“Hili limekuwa tatizo kubwa hapa nchini. Utakuta fedha zimetengwa kwa mradi fulani, badala yake wanabadilisha matumizi na kununua vitu ambavyo havina stakabadhi,” amesema Profesa Assad.

“Lengo kuu la fedha hizo za miradi ni kutumika katika shughuli za maendeleo na kutoa huduma muhimu za kijamii.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here