Mkazi wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Jaribu Obed mwenye miaka 26 amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na kosa la kumuingilia mkewe kinyume na maumbile.
Hakimu Mkazi wa mahakama ya wilaya hiyo Erick Marley amesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo bila kuacha shaka kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Alisema ametoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwake na wanaume wengine wanaokusudia kutenda kosa kama hilo
Mwendesha mashtaka wa polisi Peter Makala alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kati ya Mei 28 na 30 usiku katika kijiji cha Kumuhama.
Alidai mshtakiwa huyo alimfanyia kitendo hicho mkewe huyo kwa siku tatu mfululizo wakati akiwa na mimba ya miezi saba
Alidai kitendo hicho kilimuathiri kiafya na kukosa uvumilivu hivyo kutoroka na kwenda kutoa taarifa kwa dada yake anayeishi mtaa wa Migombani mjini Kibondo.
Mwendesha mashtaka huyo alidai baada ya dada yake kupata taarifa hizo alimpeleka katika ofisi za ustawi wa jamii kisha polisi na ambako alipewa fomu namba tatu PF3 ili kwenda kutibiwa hospitali
No comments:
Post a Comment