OFISI HABARI WA KLABU YA SIMBA BW. HAJI MANARA APOTEZA UWEZO WA KUONA. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, July 6, 2016

OFISI HABARI WA KLABU YA SIMBA BW. HAJI MANARA APOTEZA UWEZO WA KUONA.


Kunastori inazidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai Ofisa Habari wa klabu ya Simba Bw. Haji Manara amepoteza uwezo wa kuona. Taarifa zinadai awali jicho lake moja lilipoteza kabisa uwezo wa kuona na akapanga kukutana na mtaamu wa macho ili kupata ufumbuzi wa tatizo linalomkabili.

Taarifa nyingine zimetoka usiku huu (Julai 5) kwamba jicho ambalo lilikuwa linauwezo wa kuona, nalo limepoteza uwezo huo na kumfanya Manara asione kabisa kwa macho yake mawili.

Mdau wa Michezo Shaffih Dauda naendelea kutafuta ukweli wa taarifa hii ikiwa ni pamoja na kumpigia simu Manara ili athibitishe kama taarifa hizi ni za kweli au ni uvumi wa mitandaoni. Tutaendelea kukujuza kadiri tutakavyopata taarifa rasmi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here