Polisi katika mji wa Munich nchini Ujerumani wamesema mtu aliyewapiga risasi na kuwaua watu tisa katika eneo lenye maduka mengi siku ya Ijumaa hakuwa na uhusiano wowote na kundi linalojiita la Islamic State.
Wanasema kijana huyo aliyekuwa na silaha mwenye umri wa miaka 18 alizaliwa na kulelewa Munich na alikuwa na pasipoti mbili ya Kijerumani na ya Ki-Iran.
Baada ya chumba chake kupekuliwa imegunduliwa kuwa alikuwa na kama shauku kwa kile walichoita mashambulio ya kiwazimu.
Pia alikuwa anapata matibabu ya maradhi ya akili.
Polisi wamesema shambulio hilo lilikuwa na kila ishara ya mtu muuaji ila hamna uhusiano wowote na ugaidi.
No comments:
Post a Comment