POLISI YATEKETEZA SHEHENA ZA BANGI. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, July 2, 2016

POLISI YATEKETEZA SHEHENA ZA BANGI.


JESHI la Polisi, Mkoa wa Arusha limeteketeza hekari tisa za dawa za kulevya aina ya bangi zilizokuwa zimepandwa shambani.

Taarifa ya kuteketezwa kwa bangi hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, DCP Charles Mkumbo, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake mjini hapa.

Alisema bangi hiyo ilikuwa imepandwa katika mashamba yaliyo eneo la Kisimiri juu, Wilaya ya Arumeru.

Kamanda Mkumbo alisema sambamba na kuteketeza bangi hiyo, waliteketeza pia gunia 267 ya bangi yenye uzito wa kilogramu 17,355, zilizokutwa kwenye baadhi ya nyumba za wakazi wa kata hiyo.

“Katika operesheni yetu iliyofanyika Juni 29 na 30 mwaka huu tukishirikiana na vyombo vingine vya usalama, tumefanikiwa kuteketeza shehena hiyo ya bangi.

“Pia tulikamata misokoto 1,400 ya bangi yenye uzito wa kilogramu 1.5, lakini hakuna aliyekamatwa hadi sasa kwa sababu wakazi wa eneo hilo walikimbilia milimani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here