RAIS WA ZAMANI MATATANI ARGENTINA - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, July 1, 2016

RAIS WA ZAMANI MATATANI ARGENTINA


Fernandez anadaiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi
Polisi nchini Argentina wanasaka mali za Rais wa zamani wa nchi hiyo Cristina Fernandez de Kirchner.

Upekuzi unafanyika katika jimbo la kusini la Santa Cruz, kwa amri ya mahakama. Fernandez anadaiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini humo.

Hii ni kwa mara ya pili familia ya Rais huyo wa zamani kuvamiwa kwa sababu hiyo.

Mwaka jana Hoteli pamoja na baadhi ya majengo yalifanyiwa upelelezi mkali na wana usalama wa nchi hiyo.

Fernandez anamtuhumu Rais wa sasa Mauricio Macri kuwa anafanya mchezo mchafu wa kisiasa juu yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here