MJADALA WA SAKATA LA LUGUMI WAZIKWA RASMI ... NAIBU SPIKA AIPA SERIKALI MIEZI MITATU. - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, July 1, 2016

MJADALA WA SAKATA LA LUGUMI WAZIKWA RASMI ... NAIBU SPIKA AIPA SERIKALI MIEZI MITATU.


Kiu ya wabunge kujadili sakata la utekelezwa mbovu wa mkataba baina ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enteprises Limited, imezimwa baada Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuiagiza Serikali kukamilisha utekelezaji wa mradi huo ndani ya miezi mitatu ijayo. 

Kwa muda mrefu, wabunge walikuwa wakisubiri ripoti ya uchunguzi kutoka Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC) ili waweze kujadili kwa kina sakata hilo linalohusisha mradi wa Sh37 bilioni wa kufunga vifaa vya kielektroniki vya kuchukua alama za vidole (AFIS). 

Mapema Aprili mwaka huu, wakati PAC ikipitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka ulioshia Juni 30, 2014 ilibaini kuwa Lugumi ilikuwa imefunga mashine katika vituo 14 tu kati ya 108 ilivyotakiwa kuvifunga wakati ikiwa imeshapokea asilimia 99 ya malipo yote.

PAC ilimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani apeleke taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ambayo aliipeleka Aprili 18 na kubaini kuwa vifaa hivyo vilifungwa katika vituo 153 pamoja na makao makuu ya polisi. 

Kutokana na utofauti wa takwimu za CAG na PAC iliunda kamati ndogo kufanya uhakiki wa vifaa vya AFIS na sababu za kuchelewa kutekelezwa kwa mradi, huku wengi wakitarajia ripoti hiyo ingejadiliwa bungeni. 

Katika sakata hilo, wabunge walimtuhumu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kuwa na masilahi kwa madai kuwa alikuwa mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Infosys iliyoshirikishwa kwenye mradi huo na kushinikiza ajiuzulu kupisha uchunguzi. 

Hata hivyo, Kitwanga alitimuliwa kazi kwa kosa jingine la kuingia bungeni kujibu maswali ya wizara yake akiwa amelewa. 

Jana, Dk Tulia alitumia kanuni 117(17) kukabidhi matokeo ya uhakiki huo kwa Serikali, yakiwemo maoni, ushauri, mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zilizoanishwa na taarifa ya kamati ya PAC na kutoruhusu mjadala kwa wabunge

Dk Tulia alieleza kuwa amefanya uamuzi huo baada ya kupokea taarifa hiyo na kuangalia maudhui yake, kuzingatia matokeo ya uhakiki huo uliofanywa na kamati ndogo na PAC kujiridhisha uwepo wa vifaa hivyo, ukiacha kasoro zilizojitokeza. 

Pia, alisema suala hilo si jipya kwa kuwa linatokana na hoja ya ukaguzi wa miaka ya nyuma na kilichokuwa kimebaki ni vifaa hivyo kufanya kazi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here