UMOJA WA MATAIFA UNAREJESHA MAJUKUMU YA ULINZI WA USALAMA WA LIBERIA KWA POLISI - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, July 2, 2016

UMOJA WA MATAIFA UNAREJESHA MAJUKUMU YA ULINZI WA USALAMA WA LIBERIA KWA POLISI


Umoja wa Mataifa unarejesha majukumu ya ulinzi wa usalama wa Liberia kwa polisi wa taifa hilo.

Vikosi vya ulinzi vya Umoja wa Mataifa vimekuwa katika majukumu ya kuhakikisha utii wa sheria katika taifa hilo la Afrika Magharibi kwa takribani miaka 13.

Katika kipindi hicho taifa hilo lilivurugwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo maelfu ya watu waliuwawa na wengine waliachwa bila ya makazi.

Umoja wa Mataifa ulionekana mdhamini wa kuaminika wa usalama katika kipindi ambacho kitu pekee kilichokuwa miongoni mwa makabila ni hali ya kutoaminiana.

Lakini janga la ugonjwa wa Ebola la hivi karibuni liliyaweka makundi hayo pamoja na kupunguza hali ya kutofautiana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here