Wabunge wa Conservative wanafanya uchaguzi wao wa kwanza kumtafuta kiongozi mpya wa chama hicho.
Wagombea watano wanawania kumrithi David Cameron ambaye alijiuzulu baada ya kupoteza kwenye kura ya maoni kuhusu unachama wa Uingerzea kwa muungano wa ulaya.
Mgombea mkuu ni waziri wa mambo ya ndani Theresa May ambaye ametangaza uungwaji mkono wa zaidi ya wabunge 100.
Wapinzani wake wanasema kuwa kama mtu aliyeunga mkono uingerezaa kusalia katika muungano wa ulaya hayuko katika nafasi ya kushiriki mazungumzi ya uingereza kuondoka EU.
Wengine wanaowania ni Andrea Leadsom, Michael Gove, Stephen Crabb na Liam Fox
No comments:
Post a Comment