Moto mkubwa wateketeza mapipa ya lami wilayani Kilosa yaliyokuwa yamehifadhiwa katika ofisi za ujenzi wilayani humo huku jitihada za jeshi la polisi na wananchi za kuokoa mapipa hayo zikigonga mwamba licha ya kufanikiwa kuudhibiti moto kutoteketeza karakana ya ofisi hiyo.
Wakizungumza na ITV mashuhuda wa tukio hilo wamesema wameshangazwa na kuibuka kwa moto huo ambao wameeleza chanzo cha moto huo na jinsi walivyofanikiwa kuokoa magari mabovu yaliyokuwa jirani na moto huo.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo kesi Mkambara wamewashukuru wananchi kwa ushirikiano walionyesha katika kuokoa mali za serikali.
No comments:
Post a Comment