Takriban wahamiaji 126 wameripotiwa kupotea baada ya mashua walimokuwa ndani kuzama katika pwani ya bahari nchini Libya .
Taarifa hiyo imearifiwa na shirika la masuala ya uhamiaji (IOM) mapema siku ya Jumanne. Wakati huo huo msemaji wa IOM alifahamisha kwamba wahamiaji wanne waliweza kuokolewa. Wengi wa wahamiaji hao ni raia wa Nigeria na Sudan .
Shirika la uhamiaji la UN lafahamisha kwamba takriban wahamiaji 44,209 wameingia Ulaya mwaka 2017 ,wengi wao wameenda Italia ,Ugiriki,Uhispania na Cyprus. Wahamiaji wasiopungua 966 wamezama na kupotea katika bahari ya Mediterania katika njia inayounganisha Afrika kaskazini na Italia
No comments:
Post a Comment