Katika
kipindi cha mzunguko (siku za hedhi) kwa kawaida wanawake hupoteza
kiasi cha damu pamoja na baadhi ya madini chuma mwilini.
Hali
hiyo huweza kusababisha upungufu wa damu kama mwanamke atakuwa hapati
lishe bora na ya kutosha. Sasa ili kuzuia upungufu wa damu na madini
mwilini, msichana anatakiwa kula vyakula vyenye madini chuma na chokaa
kwa wingi ikiwa ni pamoja na hivi vifuatavyo:-
Orodha ya vyakula vinavyopendekezwa
Mboga za majani
Maharage
Soya
Samaki
Maziwa
Korosho
Mayai
Dagaa n.k.
Mbali
na vyakula hivyo, pia mwanamke huhitaji kuzingatia hali ya usafi wa
mwili, hasa sehemu za siri . Tumia vitambaa safi vilivyo nyooshwa kwa
pasi au pedi zilizohifadhiwa katika hali ya usafi
No comments:
Post a Comment