Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani.
Wananchi hao walitoa ushauri huo jana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la bukombe mh. Dotto biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa namna alivyosimamia sekta ya madini,mkutano ambao ulihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh.Costantine Kanyasu.
Akiwahutubia wananchi,Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko,alisema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli si ya lelemama,huku Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh. Kanyasu akisema serikali ya awamu ya tano haiwachukii wawekezaji, bali inawachukia waporaji wa raslimali za nchi.
Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini wa Makinikia,iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof.Nehemiah Ossoro ilibaini taifa kupoteza shilingi Trilioni 252 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia mwaka huu,huku ikiwahusisha baadhi ya mawaziri wa zamani wa nishati na madini waliohusika kuingia mikataba mibovu iliyoisababishia serikali hasara
No comments:
Post a Comment