RUVU SHOOTING YAICHOKONOA SIMBA KIMTINDO SOMA ZAIDI KUJUA.... - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, September 3, 2019

RUVU SHOOTING YAICHOKONOA SIMBA KIMTINDO SOMA ZAIDI KUJUA....

UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa msimu huu wa mwaka 2019/20 wamejipanga kuushangaza ulimwengu wa mpira kwa kutwaa kombe la ligi lililo mkononi mwa Simba.

 Ruvu Shoting ilishinda mchezo wake wa kwanza mbele ya Yanga ikiwa ugenini kwa ushindi wa bao 1-0 na kuvunja rekodi iliyodumu kwa muda wa misimu 9 ambapo Ruvu Shooting ilikutana na Yanga mara 18 na ilipoteza jumla ya mechi 15 na sare tatu.

Bao pekee lililoipa ushindi Ruvu Shooting lilipachikwa kimiani na Sadat Mohamed akimalizia pasi ya Hassan Dilunga, uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa wamejipanga kufanya maajabu ambayo yatashangaza ulimwengu kwa kutwaa kombe la ligi.

“Hapa hakuna cha Simba wala Yanga, kazi ndo imeanza kwa sasa hawa Yanga tuliwaambia wameponzwa na ubishi wao ni salamu kwa walioshikilia ubingwa kwamba mwendo wetu mpaka tunautwaa ubingwa msimu huu,” amesema Bwire.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here