YANGA YAMKINGIA KIFUA MRITHI WA MAKAMBO JANGWANI - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, September 3, 2019

YANGA YAMKINGIA KIFUA MRITHI WA MAKAMBO JANGWANI


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mchezaji wake David Molinga ‘Mwili Jumba’ sio wa kawaida ana vitu vya kipekee ambavyo ataonyesha mbele ya ligi.

 Molinga ni mshambuliaji mpya wa Yanga amejiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea timu ya AC Lega ya Congo amechukua nafasi ya Heritier Makambo aliyetimkia AC Horoya.

Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa,kushindwa kufunga kwa mchezaji haina maana hajui bali ni mazingira kumkataa na kukosa utulivu kwakwe kunamponza.

“Nina amini Molinga atafanya mambo makubwa ndani ya timu hasa ukizingatia tayari ameshaanza kuzoeana na wachezaji wenzake kilichobaki ni kuona matokeo kwake.

“Ligi ina michezo mingi hauwezi kutoa hukumu kwa kutumia mchezo mmoja hiyo sio sawa bado ana nafasi ya kufanya vizuri na uwezo wake utakuwa wazi kama ilivyo mchezo wa mpira akipata utulivu na mazoezi atakuwa vizuri kama ilivyokuwa kwa Makambo” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here