Mwonekano mpya wa Nizar Khalfan baada ya kukata rasta zake na kuzibakiza chache sehemu ya nyuma ya kichwa (karibu na shingo). Nizar alidumu na rasta zake ambazo alianza kuzifuga miaka 12 iliyopita kabla ya kuamua kuzikata mwaka huu
Kama ulikuwa hujui basi mimi nakujuza, na hii ni fursa ya pekee kwa wadau wa soka kujua kwamba Star wa soka la Bongo Nizar Khalfan ameamua kukata rasta zake ambazo alidumu nazo kwa muda wa miaka 12.
Nyota huyo wa zamani aliyeichezea klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada, ameiambia shaffihdauda.co.tz sababu za yeye kufanya hivyo na haikuwa kitu rahisi kuchukua uamuzi huo.
Kwanini Nizar ameamua kuzikata rasta zake?
shaffihdauda.co.tz: Kutokana na muda uliokaa nazo inaonekana ilikuwa ni vigumu sana kuchukua uamuzi wa kuzikata nywele zako ambazo zilikuwa ndefu na zilikuwa ni kitambulisho chako. Kwanini umezinyoa?
Nizar: Yeah ni maamuzi magumu sana ila napumzika kaka, ni muda sana miaka kumi 12 imepita ninazo.
Nimeamua kuzikata ili nipumzike kidogo nilikua napata tabu sana muda nikienda kusali, muda mwingine nikiwa natawadha nikiweka maji kichwani zilikuwa zinatoka nilikuwa sipendi kila mtu ajue ninanywele ndefu japokua wengi walikua wanashangaa wakiona nimevaa kofia walikua wanajua nimekata
Na nimekaa nazo muda mrefu sana. Pia nilikuwa nataka nionekane mtu mpya mbele za watu maana nimeshazoeleka na minywele.Mwonekano wa Nizar kabla ya kukata rasta zake
shaffihdauda.co.tz: Miaka 12 ni muda mrefu sana, kwahiyo hata watoto wako walikua hawajawahi kukuona katika muonekano huu?
Nizar: Yeah ni kweli kaka.
shaffihdauda.co.tz: Baada ya kuzinyoa unajisikiaje sasahivi bila nywele kwasababu umeishi nazo kwa miaka mingi
Nizar: Hahhahaha, najiskia fresh sana niko huru mnoo tofauti na mwanzo.
Rasta zilikuwa zinampa changamoto gani kwenye maisha yake ya kila siku?
shaffihdauda.co.tz: Pole sana na hongera sana kwa uamuzi wako maana nadhani sasa uko huru kuingia popote bila kujishtukia kama ulivyosema ulikuwa unapata wakati mgumu ukienda kuswali.
Nizar: Yeah ni kweli, watu wengine nilikua nakutana nao msikitini wakinikuta nipo kawaida walikua wanashangaa wanajiuliza kumbe kijana ana rasta ndefu msikitini hajulikani kabisa daah! Nilikua sijisikii vizuri, ila sasa hivi niko poa kabisa.
Mama watoto wake amechukuliaje uamuzi wa mumewe kunyoa rasta?
shaffihdauda.co.tz: Safi sana kaka, vipi shemeji amesemaje ulipoamua kunyoa nywele zako?
Nizar: Kafurahi sana na nilipoanza kunyoa alikuwepo na ndiyo alinimalizia kunyoa baada ya kuanza kukata mojamoja. Na sikuamini kama nazikata kweli.
shaffihdauda.co.tz: Alikua hazipendi?
Nizar: Hamna alikua anazipenda ila si unajua inafika mahali hata yeye aliniunga mkono nipumzike kidogo maana ni mda sana kaka.
June 21 Nizar alikuwa anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday), shaffihdauda.co.tz inamungana na wadau wengine kumpongeza na kumtakika kila kheri nyota huyo ambaye ni alama kubwa kwenye soka la Tanzania kutokana na mchango wake mkubwa usiopimika kwenye timu ya taifa sambamba na vilabu alivyovichezea.
No comments:
Post a Comment