Baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland, kocha wa Belgium Marc Wilmots amesema ilibidi azungumze na Lukaku juu ili kumjengea kujiamini na kumfanya ajione anaaminiwa na kocha wake hali iliyomfanya afunge bao mbili kwenye mchezo wa dhidi ya Jamhuri ya Ireland.
“Umoja ni muhimu. Tunashinda na kushindwa pamoja,” amesema kocha wa Belgiam Marc Wilmots baada ya mchezo.
Tulitaka kumfanya Romelu Lukaku ajiamini, nadhani amefunga magoli manne kwenye mechi nne lakini aliposhindwa kufanya hivyo kwenye mechi dhidi ya Italy kila mtu aliongea lake. Nilijarimu kumwelekeza baadhid ya vitu na kumfanya aone namuamini . Leo amefanya kile nichotarajia.”
Romelu Lukaku amefunga magoli mawili ushindi ulioifanya Belgium kuandika ushindi wa kwanza kwenye michuano ya Euro 2016 na kufifisha ndoto za Jamhuri ya Ireland kufuzu kucheza hatua ya 16 bora.
Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila kufungana, Lukaku alifunga goli lake la kwanza kwenye mashindano kwa mkwaju alioupiga akiwa nje kidogo ya eneo la hatari.
Axel Witsel akapiga bao la pili kabla ya Lukaku kuongeza bao la tatu lililotokana na shambulizi la counter-attack.
Matokeo hayo yanaiweka Belgium nafasi ya pili katika Kundi E wakiwa na pointi tatu huku wakitarajia kucheza dhidi ya Sweden kwenye mchezo wao wa mwisho wakati Jamhuri ya Ireland wo watakuwa na kibarua cha kupambana na Italy.
Dondoo muhimu
- Jmhuri ya Ireland bado hawajapata ushindi kwenye michuano ya tangu walivyoifunga England kwenye mchezo wao wa kwanza kwenye michuano hiyo mwaka 1988 (D2 L5).
- Kelvin de Bruyne amesaidia kupatikana kwa magoli 10 kwenye mechi 10 alizoichezea Belgium (amefunga magoli matano na ku-assist matano).
- Lukaku amekuwa mchezaji wa kwanza wa Belgium kufunga magoli mawili kwenye michuano mikubwa tangu Marc Wilmots alipofanya hivyo kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 1998 dhidi ya Mexico.
- Jamhuri ya Ireland imefanikiwa kucheza mchezo mmoja pekee bila kuruhusu bao kwenye mechi nane zilizopita dhidi ya Belgium.
- Axel Witsel ameifungia Belgium goli la kwanza tangu September 2014 dhidi ya Australia (sawa na siku 653 zilizopita)
- Jamhuri ya Ireland imeshindwa kupiga shuti lililolenga goli kwa mara ya kwanza kwenye michuano mikubwa tangu 1994 dhidi ya Norway kwenye fainali za kombe la dunia.
- Ushindi wa Belgium wa magoli 3-0 unawakumbusha Belgium mwaka 1970 ambapo walipata ushindi mkubwa kama huo kwenye michuano ya kombe la dunia dhidi ya El Salvador.
No comments:
Post a Comment