Mshambuliaji wa timu ya taifa ya England na klabu ya Leicester City Jamie Vardy amesaini mkataba wa miaka minn wa kuendelea kuitumikia klabu yake.
Vardy (29), ambaye alikuwa akiwaniwa vilivyo na klabu ya Arsenal amaeamua kubaki klabuni hapo baada ya kuwa msimu kiwango bora na kusaidia kuipa Leicester msimu uliopita.
“Pande zote mbili zinatumaini kwamba tangazo hili limaliza tetesi zote juu ya Jamie’s future,” taarifa ya klabu imeeleza.
Hapo awali iliripotiwa kwamba, Vardy alikuwa kwenye hatihati ya kusajiliwa Arsenal kwa ada ya paundi milioni 20 kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro inayofanyika nchini Ufaransa.
Inaaminika kwamba endapo Arsenal wangemsajili wangekuwa wakimlipa paundi 120,000 kwa wiki.
Leicester nao walirudisha majibu na kusema wao wangemlipa mshahara wa paundi 100,000.
Vardy, ambaye alijiunga na ‘the Foxes’ akitokea Fleetwood Town kwa ada ya Euro milioni 1 mwaka 2012, alikuwa tayari amesaini makataba wa miaka mitatu na Leicester mwezi Februari mwaka huu.
Kwa sasa yupo na timu yake ya taifa ya England inayoshiriki michunao ya Euro nchini Ufaransa ambapo alifunga goli katika mchezo ambapo England iliifunga Wales magoli 2-1 katika hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment