Hatua ya makundi ikiwa nyuma yetu, na timu zilizofuzu kwenda hatua ya mtoano zikiwa zishajulikana hebu tutizame takwimu bora zaidi zilizojitokeza katika hatua ya makundi Euro 2016.
- Magoli 49 chini ya 69 yaliyofungwa Euro 2016 yamefungwa kipindi cha pili 27.5% yamefungwa dakika ya 80 kuendelea na magoli mengi zaidi (3) yamefungwa dakika ya 92 ya mchezo kushinda dakika kumi za mwanzo
- Timu ya Ufaransa imeongoza kwa jumla ya dakika 17 pekee katika mechi zao tatu Euro 2016.
- Wachezaji 12 wa timu ya Liverpool na wachezaji 12 wa timu ya Juventus wanaoshiriki Euro 2016 wote wamefanikiwa kufuzu kwenda hatua ya mtoano na timu zao.
- Italy na Spain zitakutana kwa mara ya nne mfululizo katika Euro 3 pale zitakapo cheza kwenye mechi yao ya hatua ya mtoano.
- Cristiano Ronaldo aliweza kuweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi kwenye michuano ya Euro (17) alipocheza dhidi ya timu ya Hungary kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya makundi.
- Timu 9 kati ya 24 zimemaliza hatua ya makundi bia kufungwa 3 ya hizo zimetokea Group F.
- Kevin De Bruyne (17), Dimitri Payet (14) na Mesut Ozil (12) ndiye wachezaji waliongoza kwa kutengeneza nafasi za magoli.
- Kutokana na mpangilio wa mechi hatua ya mtoano fainali ya Euro 2016 ina hakika ya kuchezwa na angalau timu moja ambayo haijawahi kushinda kombe hili.
- Wachezaji wa timu ya Iceland walishangilia na asilimia 8 ya wananchi wake wote walipofunga goli dhidi ya Austria liliowapa ushindi na kuwapeleka kwenye hatua ya mtoano.
- Asilimia 50 ya matokeo ya ushindi ya timu wa timu ya Ireland kwenye michuano mikubwa iliowahi kushiriki ni matokeo ya ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Italy.
- Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye michuano ya Euro minne tofauti.
- Kipa wa timu ya Hungary Gabor Kiraly, 40, ndye mchezaji mzee zaidi kuwahi kushiriki michuano ya Euro.
- Kichapo cha 2-1 dhidi ya Croatia ni kichapo cha pili tu ambacho mchezaji Alvaro Morata amewahi kupokea kwenye mechi ambayo amefunga baada ya kile cha 2-1 dhidi ya Barcelona kwenye fainali ya ligi ya mabingwa.
- Spain wamekosa penati zao 4 kati ya 7 za mwisho walizopiga kwenye michuano ya Euro.
- Petr Cech kafungwa magoli 20 kwenye michuano ya Euro zaidi ya mchezaji mwingine yeyote kasoro Peter Schmeichel aliyefungwa 21.
- Portugal ndiye timu pekee ambayo imefuzu kwenda hatua ya mtoano bila kushinda mechi hata moja.
- Zlatan Ibrahimovic alipiga shuti moja tu katika mechi zake tatu Euro 2016.
- Katika mechi kati ya Ujerumani na Northern Ireland Toni Kroos alifikisha pasi nyingi zaidi (111) kushinda timu nzima ya Northern Ireland(105).
- Belgium walipiga pasi 28 kabla ya kufunga goli lao dhidi ya Ireland, hii ni idadi kubwa zaidi ya Pasi zilizozalisha goli tangia Euro 1980.
- Kwenye mechi dhidi ya timu ya Portugal Iceland iliweka rekodi ya michuano ya Euro ya kuwa timu yenye ‘possession’ ndogo zaidi (27.8%) bila kufungwa mechi.
- Kichapo dhidi ya Croatia kilikuwa kichapo cha kwanza cha timu ya Spain kwenye mechi ya Euro ambayo waliongoza.
No comments:
Post a Comment