INAFAHAMIKA wazi kuwa Joti na Masanja mkandamizaji ni marafiki ,na zaidi ya urafiki huo pia wanafanya kazi katika sekta moja ya burudani kupitia maigizo ya vichekesho.
Lakini linapokuja suala la maisha binafsi Joti na Masanja utofauti wao haunzia katika hili,ambapo jana kupitia mitandao mbalimbali Ilionekana Masanja akimvisha pete ya uchumba mpenzi wake MONICA ikiwa ni hatua za wawili hao katika kujihalalisha kidini.
Sasa,muda mfupi baada ya tukio hilo kusambaa na taarifa kumfikia Joti, Joti aliamua kuandika ujumbe huu kuhusu tukio hilo katika ukurasa wake wa Twitter.
No comments:
Post a Comment