Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja (kushoto) akimkabidhi zawadi ya matairi ya gari, aliyekuwa mkuu wa gereza la mahabusu la Keko, Kamishna Msaidizi Mbwana Senashinda (wa pili kushoto) baada ya kutumikia jeshi hilo kwa miaka 34 mpaka jana alipoagwa. Kulia ni mkewe Vailet Mkilanya na maofisa wa Magereza. (Picha na Yusuf Badi).
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja amewataka askari wa jeshi hilo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi huku wakitumia vyema fedha za Serikali.
Alisema hayo jana katika hafla ya kuwaaga watumishi wawili wa jeshi hilo. Kamishna Minja alisema ili jeshi hilo lifanye kazi zake kwa weledi ni lazima waongozwe na msingi mkuu wa sheria, taratibu na kanuni hizo.
Aliwapongeza askari wa jeshi hilo kwa kufanya hafla hiyo bila kutumia fedha za serikali bali kwa kuchangishana wenyewe ili waweze kuwaaga askari hao ambao wametumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 35 katika nafasi mbalimbali.
Maofisa hao walioagwa baada ya kustaafu ni Mbwana Senashida ambaye alikuwa Mkuu wa gereza la Keko na Mohamed Mdelya ambao walipewa zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia kama vile mabati na vifaa vya ujenzi baada ya askari wenzao
No comments:
Post a Comment