OMOG ATUA SIMBA RASMI - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, July 1, 2016

OMOG ATUA SIMBA RASMI


Kocha Mkuu mpya wa Simba Joseph Omog amewasili alfajiri ya leo tayari kwa kujiunga na timu hiyo akiwa kocha mkuu mpya.

Omog raia wa Cameroon ametua nchini akitokea kwao Cameroon na kupokewa na katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemele na kupelekwa moja kwa moja katika hoteli atakayofikia.

Kocha huyo mpole mara baada ya kutua alishindwa kuongea lolote ikiwa ni kutii masharti ya klabu hiyo huku akiomba waandishi kuwa wavumilivu mpaka baadaye leo atakapotambulishwa rasmi na uongozi wa Simba zoezui litakalotanguliwa na kusaini mkataba.

Kutua kwa Omog ambaye awali alifanya kazi nchini ya kuipa mafanikio makubwa Azam FC kwa kuchukua taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara kunaifanya Simba kuziba nafasi ya Muingereza Dylan Kerr aliyetimuliwa katikati ya msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here