Ureno imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Poland ikiwa ni mara ya nne kwenye misimu mitano.
Ricardo Quaresma alikwamisha penati ya mwisho ya kuipa ushindi Ureno baada ya mkaju wa Jakub Blaszczykowski kuokolewa.
Robert Lewandowski alianza kuifungia Poland bao la kuongoza kwa kichwa dakika ya pili tu tangu mchezo huo uanze lakini kinda wa Ureno Renato Sanches alisawazisha badae kabla ya mapumziko.
Ureno inatarajia kukutana na Wales au Ubelgiji kwenye hatua ya nusu fainali, timu hizo zitakuna Ijumaa kwenye mchezo robo fainali.
Ureno imefika hatua ya nne bora bila kushinda mchezo katika dakika za kawaida kufuatia sare tatu kwenye hatua makundi ambapo ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi huku mchezo wao wa hatua ya 16 bora ukienda hadi dakika za nyongeza na kushinda mbele ya Croatia.
Hakuna timu yeyote iliyoweza kufika hatua kama hii bila kushinda mchezo wowote ndani ya dakika 90.
Video ya magoli yote, Poland vs Portugal
No comments:
Post a Comment