WAWA ATIMKIA KWAO - PATRICIA-TV.com

Breaking

Share daily activities and have all funs here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, July 1, 2016

WAWA ATIMKIA KWAO


Mlinzi wa kati wa Azam FC Pascal Wawa ameondoka Dar leo alfajiri kuelekea nyumbani kwao kwao Ivory Coast kwa mapumziko mafupi baada ya kurudi kutoka Afrika Kusini katika matibabu ya mguu wake.

Wawa amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akisumbuliwa majeraha ya mguu aliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho dhidi ya Esperance ya Tunisia mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex. Katika mchezo huo, beki huyo tegemeo wa Azam FC alitolewa nje ya uwanja akiwa amebebwa kwenye machela kufuatia kuumia mguu na kushindwa kuendelea na mchezo.

Wawa pamoja na Kapombe walipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi na hivi karibuni wawili hao walirejea nchini baada ya kupata matibabu na hali zao kuimarika.


Kapombe pamoja na Wawa wamekuwa chachu ya mafanikio kwenye kikosi cha Azam na huenda kukosekana kwao kuliiathiri Azam kwa namna moja au nyingine katika mbio zao za kuwania ubingwa wa msimu uliopita pamoja na harakati za kufanya vema kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here