Cristiano Ronaldo na Lionel Messi huwezi kuongelea magwiji hawa wawili bila kuwalinganisha na ni upinzani wao huu ambao umeweza kuwafanya wachezaji hawa kuwa kati ya wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea. Kila mmoja wao milele anaishi kwenye kivuli cha mwenzake. Hakika huwezi kumuongelea Messi bila mtu kumtaja Ronaldo.
Tulikumbushwa suala hili mapema mwezi huu kwenye michuano ya Euro 2016 pale beki wa Iceland Kari Arnason alipomtaja Messi ili kumkera Cristiano Ronaldo baada ya maneno ya kuudhi ya Ronaldo kuhusu timu ya Iceland.
Baada ya tukio hili wiki moja ya midahalo iifuata—Je, tunatakiwa tumuonee huruma Cristiano Ronaldo?, Je anaweza kuibeba Portugal kwenye michuano hii?—mpaka pale magoli yake mawili dhidi ya timu ya Hungary yalipowanyamazisha waongeaji wote angalau kwa muda. Siku kadhaa baadaye Messi nae alikosa penati kwenye fainali ya Copa America dhidi ya Chile, kitendo kilichochea zaidi moto wa mdahalo kuhusu historia atayoiacha kwenye mpira, kwani fainali hiyo ilikuwa ya tatu mfululizo ambayo Messi alipoteza akichezea Argentina huku iliwa ni ya nne tangu aanze kuvaa uzi wa imu yake ya taifa. Haikuchukua muda mrefu baada ya hapo kwa Messi kutangaza kuwa amestaafu soka la kimataifa.
Matukio haya yote yamezua tena mdahalo uliozoeleka wa nani mbabe zaidi kwenye timu ya taifa. Japo wote wawili hawa wameweza kuweka takwimu za ajabu wakichezea klabu zao, ila tukija kwenye timu za taifa mambo yanakuwa magumu kidogo.
MAGOLI
Ronaldo: 60 kwenye mechi 130
Messi: 55 kwenye mechi 113
REKODI KWENYE MICHUANO MIKUBWA
Ronaldo kwenye Michuano 6: Fainali moja, nusu fainali mbili, robo fainali moja, hatua ya 16 moja, katolewa kwenye hatua ya makundi mara moja
Messi kwenye Michuano 7: Fainali 4, Robo fainali 3
MICHUANO BORA ZAIDI
Ronaldo: Hadi leo hii Euro 2004 iliyofanyika nyumbani kwao Ureno, bado inakumbukwa kama michuano iliyomtambulisha kwa dunia. Licha ya kugawa penati kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Greece , Ronaldo akiwa na miaka 19 hakutetereka hata kidogo. Alikuwa moto wa kuotea mbali kuanzia hapo, hasa kwenye robo fainali dhidi ya England alipopambana na Ashley Cole. Ronaldo pia alifunga goli muhimu la kwanza kwenye nusu fainali dhidi ya Uholanzi.
Ronaldo aliisaidia Ureno kufika adi fainali ya Euro 2004
Messi: Kombe la Dunia 2014. Japo kupewa kwake kwa tuzo ya mchezaji bora kwenye michuano hiyo kulileta gumzo kwa sababu hakucheza vizuri kwenye fainali, lakini hili lisitufanye tusahau kwamba Messi ndiye aliyeweza kuwapeleka Argentina mpaka fainali tena hakiwa hachezi kwa uwezo wake wote. Messi alifunga magoli ya ushindi mawili dhidi ya Bosnia na Iran pia ndiye aliyetoa pasi ya mwisho ya goli la ushindi ndani ya dakika za mwisho kabisa kwenye mechi ya hatua ya pili dhidi ya Switzerland. Lakini Messi hakuishia hapo kwani kwenye robo fainali, aliweza kupiga pasi ndefu ya ajabu dhidi ya timu ya Belgium na kuisaidia Argentina kupata ushindi.
MICHUANO MIBAYA ZAIDI
Ronaldo: Kombe la dunia 2010. Ronaldo alikuwa kwenye ubora wake lakini alishindwa kufanya chochote cha maana kwenye michuano hii na timu yake ilitolewa kwenye hatua ya 16 dhidi ya Spain. Goli lake kwenye ushindi wa 7-0 dhidi ya North Korea lilikuwa goli lake la kwanza la Ureno ndani ya miezi 16.
Messi: Copa America 2011. Messi alizomewa na mashabiki wake mwenyewe kwenye michuano hii. Kipindi hiki messi alikuwa akisemwa sana na watu wengi walikuwa wanajiuliza kwanini Messi hakuweza kucheza vizuri Argentina kama anavyocheza Barcelona. Alianza michuano hii vibaya akishindwa kuelewana na kipenzi cha mashabiki Carlos Tevez. Japo alichangamka kadri michuano hiyo ilivyoendelea Messi alitolewa kwenye robo fainali bila goli hata moja.
WAKATI WAO MZURI ZAIDI TIMU YA TAIFA
Ronaldo: Ronaldo alipofunga magoli yote manne kwenye mechi ya kufuzu Kombe la dunia 2014 tena akimzidi kiwango Zlatan Ibrahimovic huku akifanya hivyo. Jambo hili lilionesha kwa kiasi gani Ureno wanamtegemea Ronaldo.
Messi: Messi hajafanya kitu chochote kile ambacho kinakumbukwa zaidi lakini ana matukio mengi ambayo yanaelekea kufikia kiwango hicho. Labda kwenye mechi ya Robo fainali ya Copa America dhidi ya Paraguay alipowaaibisha wachezaji wane kwa kumuibia mmoja mpira, kuruka ‘tackle’ ya mwengine, kumpiga tobo mwingine halafu kufanya wengine wawili kugongana.
WAKATI WAO MBAYA ZAIDI TIMU YA TAIFA
Ronaldo: Alipoleta uchoyo na kujiwekea mwenyewe penati ya mwisho dhidi ya Spain kwenye mikwaju ya penati ya nusu fainali ya Euro 2012, licha ya kuwa hakufanya chochote kwenye mechi hiyo. Kibaya zaidi hakupata hata nafasi ya kupiga hiyo penati kwani Spain walishinda mapema kabisa.
Messi: Alipokunja mpira nje kidogo ya goli la Manuel Neur kwenye fainali ya kombe la dunia 2014. Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake kubwa ya kuvunja mdahalo kabisa ya nani bora zaidi. Kilichoudhi watu zaidi ni pale Messi alipomuaibisha Neur mara mbili mwaka mmoja baadaye akichezea klabu yake ya Barcelona kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Messi akikosa Goli kwenye fainali ya Kombe la Dunia 2014
TIMU BORA ZAIDI WALIYOCHEZA NAYO
Ronaldo: Euro 2004, siyo tu kwamba hii ndiyo ilikuwa timu ya Ronaldo pekee kufika fainali, bali hii timu ilikuwa ina kila kitu wakiwemo nyota wa Ureno wa Euro 2000 kama Figo na Nuno Gomes waliomwezesha kijana mdogo wa miaka 19 kunga’a. Tangu michuano hii timu zote za Ureno zilizofuata zimekuwa zenye uoga na kupenda kukaba zaidi na kumtegemea Ronaldo kupita kiasi.
Messi: Copa America 2007. Timu ya Argentina aliyochezea Messi iliyokuwa inajua kushambulia zaidi kushinda timu nyingine yeyote. Kwenye timu hii walikuwemo wakina Riquelme, Crespo, Milito, Cambiasso na wengineo.
Argentina ilikuwa ina bahati mbaya tu kwani kocha wao Alfio Basile alizidiwa mbinu kwenye fainali dhidi ya kocha wa Brazil Dunga na hatimaye kufungwa 3-0. Tangu hapo mambo hayajaweza kumkalia sawa tena Messi. Ni kati ya Kocha kutoifaa timu kama 2010 na 2015 chini ya Diego Maradona, ama wachezaji wenzake kutoonesha kiwango kizuri kama 2014 na 2016.
Maamuzi nakuachia wewe.
No comments:
Post a Comment